Mzize, Kibwana wapigwa faini Sh milioni 1

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu (TFF) limemtoza faini ya Sh milioni 1 mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize kwa kosa la kuonekana akiondoa taulo la mlinda mlango wa klabu ya Dodoma Jiji.

Taulo hilo liliwekwa kwenye lango la timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa Februari 5, 2024 uwanja wa Azam Complex.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) imefafanua kuwa adhabu hiyo imezingatia kanuni ya 41:5 kuhusu udhibiti kwa wachezaji.

Mchezaji mwingine wa timu hiyo Kibwana Shomary ametozwa faini ya Sh milioni 1 kwa kosa la kuonekana akiondoa taulo la mlinda mlango wa klabu ya Mashujaa lililowekwa pembeni ya lango wakati mchezo ukiendelea.

Kwa mujibu ya TFF tukio hilo liliashiria imani za kishirikina. Aidha wameeleza kuwa adhabu hiyo imetokana na kanuni 41:5 ya udhibiti kwa wachezaji.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments