Tutaendelea kutekeleza na kufanya shughuli mbali mbali za kuleta maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumala kwajili ya maslahi mapana ya wananchi kwa kuzingatia mahitaji kwa kujali na kuendana na wakati.
Kauli hiyo imesema na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Singida Bi. Martha Mlata katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 47 katika kataa ya Idodyandole tarafa ya Itigi Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Wa Singida Bi. Martha Mlata Ameeleza kuwa nchi imeendelea kubadilika kwa kasi hasa katika awamu hii ya Dr. Samia katika swala la maendeleo kila mahali katika nchi imepata miradi ya maendeleo kwa kujali na kuzingatia mahitaji ya jamii husika.
Aidha Bi. Mlata ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wananawapeleka watoto shule kwani sasa serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya utoaji elimu imeendelea kuwa bora nchini.
Kwa Upande Wa Mkuu Wa Wilaya Ya Manyoni Kimirembe Lwota alitoa wito kwa wabunge,madiwani na vingozi mbalia mbali kwa kushirikiana na wazai na walezi kuhakikisha watoto wanaende shule.
Kimilembe ameeleza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wazazi na walezi watakao pelekea watoto kushindwa kwenda shule.
Yohana Msita Mjumbe Wa Halmashauli kuu ya taifa kutoka mkoa wa Singida (NEC) amesema kuwa chama cha mapinduzi (CCM) ni chama kinacho simamia amani na maendeleo kwajili ya maslahi mapana ya jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa Upande wa Mjumbe Wa kamati ya Siasa mkoa wa Singida Dr. Denis Nyirah ameeleza kuwa viongozi wanao tokana na chama cha mapinduzi CCM ndio viongozo wanaojali na kudhamini wananchi kwa kuendelea kusimamia na kuleta miradi mbali mbali katika jamii na taifa kwa ujumala.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya manyoni Bw.Jumanne Ismail Makhanda amesema Wilaya ya manyoni ni salama na kazi inaendeleo .
0 Comments