RUN FOR BINTI MARATHON YAWAWEZESHA WANAFUNZI WA SEKONDARI MTWARA KUPATA VYOO SALAMA NA TAULO ZA KIKE

Kwa jitihada za pamoja kuwawezesha wasichana na kuboresha upatikanaji wa haki zao za elimu na afya bora Smile for Community na Legal Services Facility (LSF) waandaaji na waratibu wa mbio za Run for Binti wamekabidhi vyoo vyenye matundu 12 kwa shule za sekondari Nanyamba na Chawi katika Halmashauri ya mji Nanyamba pamoja na kugawa taulo za kike 2500 kwa wanafunzi wa kike ikiwa ni juhudu za wadau mbalimbali kupitia mbio za run for Binti zilizofanyika mwaka jana.


Mbio za Run for Binti zinaratibiwa kila mwaka kwa mwaka wa 3 sasa ambapo mwaka jana mbio hizi zilifanyika mwenzi wa saba kwa lengo la kuweka nguvu na rasmilimali za pamoja katika kuwawezesha watoto wa kike kupata hedhi salama na kurekebisha miundo mbinu ya shule ikiwemo kuwepo wa vyoo salama pamoja na maji ili kulinda na kuboresha hali ya wanafunzi mashuleni. Makabadhiano hayo yanafatiwa kukamilika kwa ukarabati na ujenzi wa vyoo hivyo ambapo vimeboreshwa zaidi na kuwekewa mabomba na masinki ya kunawia mikono pamoja na chumba maalumu cha kubadilishia kwa watoto wa kike. Aidha ukarabati wa vyoo umefanyika kwa vyoo vya watoto wa kiume pia

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Smile for Community bi Flora Njelekela amesema tulianzisha mbio hizi kwa lengo la kumlinda mtoto wa kike na kumpatia hedhi salama na kumwezesha kuwa na mazingira bora ya kupata elimu na kuongeza ufaulu wake darasani. Tunafahamu kwamba vyoo bora ni muhimu sana kwa ustawi na afya ya wanafunzi wetu. Kupitia ujenzi wa vyoo hivi na ugawaji wa taulo za kike kwa kila binti tunahakikisha kwamba wanafunzi wetu wanapata mazingira salama na ya kujifunzia bila kuathiriwa na magonjwa au changamoto za kukosa taulo za kike, hivyo tunajisikia furaha kupitia mbio za mwaka jana tunaziwezesha hizi shule mbili leo hii. nawaomba walimu wetu na wanafunzi kuhakikisha kwamba vyoo hivi vinatunzwa vizuri ili viweze kutumika kwa muda mrefu

Kwa upande wake Meneja Masharikiano na Mawasiliano wa LSF, Bi Jane Matinde Amesema kwa zaidi ya miaka 12 sasa LSF limejikita katika kuwezesha upatikanaji wa haki ikiwemo haki ya elimu na afya bora na ndio maana tukaona iko haja ya kushirikiana na smile community katika kuandaa na kuratibu mbio hizi kila mwaka na kuomba wadau wengine kutuunga mkono kila mwaka hivi tunajisikia fahari na hatua tuliyoifikia leo ya kumwinua mtoto wa kike na kumlinda kiafya na kielimu“

“kukamilika kwa mbio za mwaka jana ndio mwanzo wa mbio za mwaka huu hivi napenda kuchukua fulsa hii kutanga mbio za mwaka huu zitafanyika tarehe 25 mei na hivyo tunatoa wito kwa wadau mbalimbali mtu moja moja kuungana nasi na kuweka nguvu ya pamoja ili tuweze kuzifikia shule nyingi na wanafunzi wengi zaidi” aliongeza Matinde

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Afisa Tarafa wa Nanyamba Sefu Nayembe amewashukuru LSF na Smile Community kwa kuweza kukamilisha ujenzi wa Vyoo na kugawa Taulo za Kike 2500." Ninawashukuru sana kwa kuweza kugawa taulo za kike na kuboresha vyoo hivi vya wanafunzi na kuweka pia chumba cha kubadilishia taulo za kike kwa wasichana hii itawezesha wanafunzi kujifunza vizuri na kutokupata shida yoyote wawapo kwenye hedhi na kusababisha kufanya mitihani yao vizuri. Natoa wito kwa jamii kuunga mkono jutihada za Serikali kama inavyofanywa na wadau hawa leo. ".

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wote, Mwanafunzi Faima Abdallah amesema " Ninawashukuru sana LSF na Smile for Community kwa kutujengea vyoo na kugawa taulo za kike kwa ajili ya kutusaidia tukiwa kwenye hedhi hii itatusaidia sana tukiwa masomoni kufanikisha ndoto zetu pasipo kupata changamoto yoyote ile".

Mbio hizi za Run for Binti za mwaka 2023 zilidhaminiwa na Isuzu, SGA security, Total, Water for People, na Afya Water na mwaka huu wa 2024 mbio hizi zimepangwa kukimiba tarehe 25 mei jjiji Dar es saalam na fedha zitakazokusanya zitaenda kusaidia kuboresha miundo mbinu na kutoa taulo za kike kwa shule, kujenga visima vya maji, kupanda miti na kutunza mazingira na kutoa elimu ya afya na haki kwa shule zilizo pembezoni mwa nchi na zenye ukosefu wa nyenzo hizo muhimu
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Afisa Tarafa wa Wilaya Nanyamba Ndg. Seif Nayembe akikabidhi sehemu ya Taulo za Kike 2500 zilizokabidhiwa kwa wanafunzi wa Kike wa Shule ya Sekondari Nanyamba. Pembeni ni Bi. Jane Matinde kutoka LSF, Bi Flora Njelekela kutoka Smile For Community na Bi. Doreen Dominic kutoka Stanbic Bank.
Kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Afisa Tarafa wa Nanyamba Ndg. Seif Nayembe akiwa kwenye picha ya pamoja wawakilishi kutoka LSF, Smile For Community, Stanbic Bank, walimu na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Nanyamba, mara baada ya Uzinduzi wa Vyoo vilivyokarabitwa kutokana na ufadhili wa Mbio za Run For Binti.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments