LIGI Kuu nchini Italia ‘Serie A’ itasalia na timu 20 baada ya vilabu 16 vya sasa kupiga kura ya kupinga kupunguzwa hadi 18.
Juventus, Inter Milan, AC Milan na Roma pekee ndio waliopigia kura pendekezo la kupunguza idadi ya timu kwenye mkutano wa wanahisa huko Milan.
Muundo wa sasa wa timu 20 ulianzishwa mnamo 2004-05.
Pendekezo la mageuzi pia liliidhinishwa huku ligi ya Italia ikishinikiza kujitawala zaidi, sawa na Ligi Kuu ya Uingereza.
Marekebisho hayo yatawasilishwa katika mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka la Italia (FIGC) mwezi Machi.
“Kwa sasa, mfumo hauipi Serie A uhuru na uzito wa kufanya maamuzi ambayo inapaswa kuwa nayo kuhusiana na uzito wa kiuchumi,” Rais wa Serie A Lorenzo Casini alisema.
0 Comments