Serikali kuanzisha somo uchambuzi wa michezo

SERIKALI imesema inatarajia kuanzisha somo la uchambuzi wa habari za michezo katika vyuo vinavyofundisha masomo ya uandishi wa habari kama ambavyo tayari imekwishaanza mchakato wa kuhakikisha chuo cha michezo cha Malya kinakuwa na mtaala wa kufundisha uchambuzi wa michezo kwa ajili ya kuongeza mtaala wa uchambuzi wa habari za michezo.

Hayo yameelezwa leo, Februari 2,2024 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo Lushoto, Rashidi Shangazi aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kuendeleza wachambuzi wa soka ili wawe na utaalamu wa kutosha katika kazi hiyo.

Naibu Waziri, Mwinjuma amesema Serikali itajadiliana na vyuo vinavyofundisha masomo ya uandishi wa habari kwa ajili ya kuongeza mtaala wa uchambuzi wa habari za michezo na kuwatumia waandishi wa habari za michezo wanaofanya shughuli za uchambuzi wa michezo kwa umahiri na weledi kama sehemu ya wanaotoa mafunzo kwa ajili ya waandishi wengine wanaotaka kujifunza kuchambua habari za michezo.

“Uchambuzi katika michezo ni sehemu ya mada zinazohusiana na michezo husika ambazo zipo katika sheria zinazotawala michezo. Serikali itaangalia mahitaji ya soko katika kipindi cha kuhuisha mitaala na kuzingatia eneo la uchambuzi ambalo sasa limeiletea heshima michezo kupitia wachambuzi nguli na mahiri waliopo” amesema Mwinjuma

Aidha Naibu Waziri Mwinjuma amesema aomo hilo halitahusisha soka pekee bali michezo mingine ikiwemo Ngumi, ambayo ni miongoni mwa michezo inayotangaza vyema Taifa la Tanzania na kutoa fursa za ajira.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments