Serikali Kufanya Maboresho Ada Leseni Za Madaktari

SERIKALI imesema itafanya maboresho ya ada za leseni za madaktari chini ya Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT).

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa taarifa hiyo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi uliofanyika jijini Dodoma.

Waganga hao walitoa ombi kwa Serikali kuona namna ya kupunguza gharama za leseni za udatkari wanazotakiwa kulipa.

“Ada mlikuwa mkilipa kila mwaka Sh100,000 na sasa hivi mnalipa Sh 150,000 kwa miaka 2, tumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alituelekeza tupunguze angalau imepunguza kwa kiasi na dhamira ya Serikali mmeiona kwa kupunguza ada za leseni lakini mimi na Naibu Waziri Mhe. Godwin Mollel tutaendelea kuwabana Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na wa OR-TAMISEMI ili tuzidi kupunguza zaidi”. amesema Waziri Ummy.

Ummy ameitaka MCT kutekeleza mipango ikatayowanufaisha zaidi wanachama wake ambao ni madaktari kwa kuwa na mikakati endelevu ikiwemo kuwaendeleza kimasomo ikiwemo ubingwa na ubingwa bobezi pamoja na mafunzo ya muda mfupi.

Aidha amemuelekeza Naibu wa Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel kukaa na MCT kuangalia makusanyo na matumizi yao ili kuja na mpango kazi wa matumizi ya fedha hizo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments