Serikali kujenga kituo cha mabasi Mkaneledi

SERIKALI imetoa pesa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mkanaledi kilichopo kata ya Magomeni Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.

Akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, Shadida Ndile amesema mradi huo unatekelezwa kupitia mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya miji nchini (TACTIC).

Kikao hicho ni kuhusu kujadili taarifa ya halmashauri hyo robo ya pili kwa mwaka 2023/24 kilichofanyika kwenye manispaa hiyo.

Aidha, amewataka viongozi kwenye manispaa hiyo kuwashirikisha wananchi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inakwenda kutekelezwa kupitia mradi huo.

Licha ya ujenzi wa kituo hicho lakini mradi unaenda kutekeleza miradi mingine ikiwemo barabara inayozunguka soko la chuno.

Pia mifereji mikubwa na imara ili kuwapunguzia changamoto ya kujaa maji wananchi kwa baadhi ya maeneo kama vile kiangu,shangani na mengine.

Hata hivyo ujenzi wa jengo la wajasaliamali litakalo jengwa skoya katika manispaa hiyo ambalo litasaidia kuwakusanya vijana wote wanao jishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments