Sh bilioni 4 kutibu watoto wenye Selimundu

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa Sh bilioni 4 kwa ajili ya kuwatibu watoto 20 wa ugonjwa wa selimundu.
Hayo yamesemwa leo Februari Mosi, 2024 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu baada ya Rais Samia kutembelea hospitali ya Benjamini Mkapa na kuwajulia hali watoto watatu ambao wamepona Selimundu.

Ummy amesema Rais Samia ametoa kiasi hicho cha fedha ambacho sasa kitaenda kutibu watoto 13 kutoka idadi ya watoto saba ya awali, kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu.

Watoto waliotembelewa na Rais Samia leo ni Grace Hosea (8), Elisha John (11), na Isack Kedmond (10), ambao wamepona ugonjwa huo wa Selimundu ikiwa ni matibabu ya mara ya kwanza tangu Huduma za Upandikizaji wa Uloto ianzishwe hospitali ya Benjamini Mkapa.

Matibabu ya Upandikizaji wa Uloto yanagharimu kati ya Sh milioni 65, hata hivyo, tafiti zinaonesha kuwa, kumhudumia mtoto mwenye Seilimundu dawa za kupunguza makali ya ugonjwa, fedha hizo zinaweza kukidhi huduma kwa miaka mitano pekee.

Akizungumza na watoto hao Rais Samia amewataka kula vizuri na kuhakikisha wanazoma sana ili wawe madaktari wa Selimundu.
Rais Samia: Unaitwa nani?
Mtoto: Naitwa Elisha
Rais Samia: Kwa sasa unajisikiaje
Elisha: Nimepona, sasa hivi kila siku naenda shule tofauti na zamani nilikuwa naenda shule kwa saa tu alafu narudi hospitali.
Rais Samia: Kwa hiyo sasa hivi unaenda shule wiki inaisha, alafu unaenda tena?
Elisha: Ndio
Rais Samia: Haya nyie unapaswa ule vizuri sio mama anasema Elisha kula unasema mama mi sili sijisikii, nyie nyote mnapaswa kula na msome kwa bidii ili mje kuwa madaktari wa Selimundu hapa Benjamin Mkapa mje msaidie watoto wengine.
Aidha, Rais Samia amesema kuwa Sh bilioni 9 zimetolewa na serikali yake katika hospitali hiyo ili kuwasomesha madaktari bingwa ili waweze kutoa matibabu ya kibobezi.
Nao wazazi wa watoto hao wamemshukuru Rais Samia kwa kuwekeza fedha katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuwahudumia bure watoto wenye Selimundu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments