TABORA: SIMBA FC wamevuna pointi tatu, magoli 0-4 dhidi ya Tabora United, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora.
Shukrani kwa Pa Omary Jobe aliyeitanguliza Simba dakika 16′ kwa bao safi la kichwa.
Sadio Kanoute akawainua tena vitini mashabiki wa mnyama dakika 35′ ya mchezo na kwenda mapumziko na mabao mawili.
Kipindi cha pili dakika 59′ Che Malone Fondoh akapeleka msiba kwa wenyeji wa mchezo huku dakika 86′ Fredy Michael Koublan akiihakikishia Simba ushindi kwa kufunga bao la nne la mchezo na bao lake la kwanza tangu ajiunge na mnyama dirisha dogo la usajili.
Matokeo haya, yanaifanya Simba kufikisha pointi 29 katika michezo 12 na kusalia katika nafasi ya tatu wakati Tabora United anabaki nafasi ya 12 pointi 15 katika michezo 13 ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
0 Comments