Tanapa Yaandaa Mtoko Siku Ya Wanawake

KUELEKEA siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 2, 2024, Mamlaka za Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kushirikiana Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia(TAZARA) wanaanda mtoko maalum kwa ajili ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere kujionea vivutio vilivyopo.

Akizungumza na  waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Kamishina wa TANAPA , Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini mwa Tanzania ,Asteria Ndaga  alisema mtoko huo wa siku moja utahusisha usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam hadi hifadhini na kurudi na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali.

Amesema watakaotembelea watapata fursa ya kuingia katika hifadhi na kuona wanayama,ndege,mabwawa mbalimbali na watapata vyakula na vinywaji wakiwa ndani ya hifadhi.

“Lengo ni kuhamasisha wanawake ili kushiriki katika utalii na uhifadhi na umuhimu wake hafla itanzi Dar es Salaam na kutembelea hifadhi ya taifa Nyerere ili kwenda kuona vivutio mbalimbali vilivyopo na kutoa taarifa za vivutio vya taifa Tanzania  na kama TANAPA tunashirikiana wenzetu wa  chama cha wanawake wa TAZARA.

Amesema gharama ya mtoko huo kwa mtu mmoja ni Sh 200,000 ambapo itahusisha huduma zote ikiwemo usafiri na chakula.

Aidha katika mtoka huo amesema wanatarajiwa kuwafikia zaidi ya wanawake 400 kutoka maeneno mbalimbali huku wanaume pia wakikaribishwa kushiriki.

“Lengo ni kuona uhifadhi unaendelea  na kuhamasisha watanzania kupitia siku ya wanawake kila mmoja aone umuhimu na fursa zilizopo katika hifadhi  na wanawake katika umoja wetu tukitumia hizo fursa tutaendeleza jitihada za Rais Samia ambaye amejitoa kuhakikisha uhifadhi unaenendlea na kupia filamu ya royal tour tumeongeza wataalii”.amesisitiza.

Amesema watakaohudhuria wanatakiwa kujiandikisha kwa  kutembelea  kurasa za kijamii za TANAPA  watapata taarifa zaidi waweze kulipa.

Kwa upande wake dereva wa treni kutoka TAZARA , Judith Ligenzi amewahamasisha wanawake  kujitokeza kwa wingi  kuona kazi za wanawake wenzao kwani  wengine wanasikia kuna  madereva wanawake wanaendesha treni na wengine hawaamini.

“Niwahakikishie tupo na tunajiamini na tutaendesha treni kutoka Dar es Salaam hadi Nyerere nakurudi tukiwa salama na tumeona tutengeneze hii kwasababu reli yetu ya TAZARA inapita mbugani na watu watatumia usafiri wa treni ni kilometa 200 kufika eneo la hifadhi.

Amesema katika mtoko huo kutakuwa na wanawake kutoka makundi mbalimba kama  taasisi,mashirika,vyuoni na kuwasisitiza wajitokeze  kufurahi pamoja kwa kutumia usafiri wa treni na kutembelea hifadhi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments