Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Chifu THOMAS MGONTO amewataka wananchi kuacha kuiga Mila na Desturi za mataifa ya nje na badala yake wafuate Mila za kitanzania na kiafrika ili kuondoa changamoto ya mmomonyoko wa Maadili katika Jamii.
Chifu MGONTO alisema hayo Mkoani Singida wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, ambapo alisema baadhi ya Watu wamekuwa wakiharibu Tamaduni za kiafrika kwa kuiga Mila na Desturi za mataifa ya nje.
Alisema mmomonyoko wa Maadili katika Jamii kwa nyakati hizi unachangiwa na kuchukua Mila za kizungu zisizofaa na kuziingiza katika Tamaduni zetu.
Aidha Chifu MGONTO aliwataka Wazazi na Walezi kuhakisha wanawalea watoto wao kwa kufuata misingi ya Mila, Desturi na Tamaduni zetu za kitanzania ili kuendelea kulinda asili za mila za makabila yaliyopo nchini.
Hata hivyo alisema suala la kuiga sio baya ila tuige vitu vyenye faida katika Jamii na Taifa kwa ujumla.
0 Comments