Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo, Mbatty amesema wanafahamu fika Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri lakini maandalizi yao ni kuzisaka pointi tatu.
“Sisi kama Tabora United tumejiandaa kwenye mchezo wa kesho na tuna deni kubwa kwa wana tabora kwa sababu kila tunapocheza kwenye Mkoa wetu wanakuja kutusapoti hivyo tunajua tunaenda kufanya nini siku ya kesho hivyo tunawaomba waje kwa wingi siku ya kesho.” Amesema.
Nahodha huyo ameongeza kuwa katika mchezo wa kesho watazingatia zaidi maelekezo ya mwalimu na benchi la ufundi kwa ujumla ili waweze kuvuna pointi tatu licha ya mpinzani wake kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa fc wakiwa katika Uwanja wao wa nyumbani.
0 Comments