Ulinzi kuimarishwa uchaguzi serikali za mitaa

JESHI la Polisi nchini limesema limejipangaa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Januari 31,2024 na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Camllius Wambura wakati wa mahafali ya saba na nane ya shahada na stashahada ya sayansi na upelelezi wa makosa ya jinai yaliyofanyika katika Chuo cha Polisi Kurasini.

Aidha,IGP Wambura amesema jeshi  hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine linajiandaa kwaajili uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani nakutaka wananchi kutoa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa amani.

Pia,amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na
vyombo vingine wamejipanga kuhakikisha wanasimamia chaguzi zote kwa amani na utulivu.

“Jeshi letu linajiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwaka 2025 nitoe rai kwa wananchi wote kuishi katika falsafa ya polisi jamii wa kutoa taarifa zote viashiria vya uvunjifu wa amani kwenye maeneo yenu,”amesema kamanda Wambura.

Kauli ya Kamanda Wambura inakuja wakati joto la uchaguzi likiwa limepamba moto maeneo mbalimbali huku viongozi wa vyama vya siasa wakitoa matamko mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu mahafali hayo IGP Wambura amesema mafunzo hayo waliyoyapata yatawasaidia kutenda kazi zao kwa uadilifu kuzingatia kanuni taratibu na sheria mbalimbali ili kiepusha mgogoro baina ya taasis zilizowaajiri na wananchi

“Mkawe wasomi na sio bora wasomi na elimu mliyoipata isiwe daraja la kuwapandisha vyeo au kuongezewa mshahara bali mkawe chachu ya maendeleo na kuboresha ustawwi wa jamii Ili kujenga taswira njema kwa jeshi la Polisi na taasisi zake,”amesema

“Tambueni wajibu wenu na kujituma kwa ukamilifu mkihakikisha uhalifu haupati nafasi kwenye jamii na kupinga matendo yote yaliyo kinyuyime na maadili,”amesema Wambura

Mwenyekiti wa w bodi ya ushauri Profesa Florens luoga alisema mahafali hayo ni matokeo ya kazi nzuri ambayo imefanywa, kwa kuwa mafunzo yameendelea kuboreshwa.

Pia,mebainisha kuwa taifa linaamini kuwa wahitimu hao wamekamilika kumepokea majukumu ili waweze kutekeleza kazi zao kwa uweledi na ufanisin mkubwa zaidi.

“Mko tayari kutekeleza majukumu mtakayopewa kwasababu elimu mliyoipata na mafunzo sio yenu wenyewe, mafunzo mliyokamilihsa ni kwaajili yetu na watanzania mna wajibu wa kuyatuma kwa uadilifu makubwa kwaajili ya nchi yetu na watanzania,”amesema

Amebainisha kuwa, wanapohitimu, wanawasifi Kwa kuwa wakijituma na kufuata mafunzo kwa uwanifu na kuweka jitihada zao mbele.

“Sisi tunafurahi kwa kuwa mliweka mipango yenu na kuhakikisha mnafanikisha ndoto zenu na taifa linapata maafisa ambao wataweza kuboresha huduma za polisi nchini,”amesema

Kwa upande Mwingine, Mkuu wa wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Lazaro Mambosasa amesem kuanzishwa kamisheni ya mafunzo na utafiti itasaidia kuimarisha kazi ndani ya Jeshi la Polisi.

Amesema wataendelea kufuatilia mifumo mitandaoni Ili kila muhitimu awe na uwezo wa kufuatilia matukio mtandaoni kwani wahalifu wamewekeza kwenye teknolojia na mawasiliano wakiamini hakuna mtu anaweza kuwafuatilia

“Nikuahidi kwa kushirikiana na wenzangu tutahakikisha askari wanatenda kazi kwa weledi wa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha tunapungunguza malalamiko ya wananchi dhidi ya jeshi la Polisi,”amesema Mambosasa.

Happy mwakakusi mmoja wa wahitimu amesema atahakikisha mafunzo waliyopata anaenda kufanya kazi Kwa mujibu wa taratibu na sheria na kuepusha malalamiko dhidi ya wananchi.

Kwa upande wake Hemed Hussen, ambaye pia ni muhitimu amesema elimu aliyoipata itamuwezesha kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

“Kama kauli mbiu ya Jeshi la Polisi inavyosema haki, weledi ni msingi ndivyo nitakavyotumia haki na weledi katika kutekeleza majukumu yangu bila kumuonea au kumnyanyasa mtu ,”amesema Hussen.

Katika mahafali hayo ya saba na nane zaidi ya wahitimu 700 wamehitimu ngazi ya Stashahada na astashahada ya sayansi ya Polisi ngazi ya upelelezi wa makosa ya jinai na taaluma ya mawasiliano ya jeshi la polisi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments