Viongozi tunapaswa kuwa waaminifu na wachamungu asema Chief Thomas Mgunto mjumbe wa kamati ya siasa CCM Mkoa Wa Singida.
Hayo yamesemwa wilayani mkalama mkoani Singida Na Chief Mgunto Wakati akizungumza na vingozo mbali mbali wa chama na serikali wilayani humo.
Chief ameeleza kuwa viongozi waaminifu na wachamungu ndio viongozi wanaojenga imani na wananchi kwa kuendelea kutenda na kusimamia haki kwa kujali usawa na kuzingatia taratibu ziliwekwa na nchi.
Aidha Chief Mgonto amesema kuwa CCM ni chama chenye Viongozi wenye ufaham , waaminifu na wachamungu kwakuendelea kujali maslahi ya taifa na kuwatumikia wananchi kwa maslahi mapana ya taifa na jamii kwa ujumla.
0 Comments