Wachangia Fedha Kujenga Daraja La Muda

ULANGA, Morogoro: WANANCHI wa kata ya Mwaya iliyopo Wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro kwa kushirikiana na mbunge wamechanga fedha za ujenzi wa kivuko cha muda katika Mto Ruaha ili kurejesha huduma za kijamii na kiuchumi zilizokwama kufuatia daraja la awali kukatika.

Daraja hilo lilikatika Februari 6, 2024 kutokana na mvua zianzoendelea kunyesha. Awali ya kuharibika lilikuwa kiunganishi cha Wananchi wa Kata ya Ilonga, Ketaketa, Mbuga na Mwaya.

Mkazi wa Kata hiyo Riston Francis amesema kuwa baada ya kukatika kwa daraja lililojengwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Alaudin Hasham, Diwani, wananchi na wafanyabiashara walijitokeza kuchanga fedha za ujenzi wa daraja la muda.

“Tunatoa shukrani za dhati kwa viongozi kususani Mbunge na diwani wametoa fedha sh milioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la muda na litakamilishwa kwa wakati ili litumike,“ amesema Francis.

Naye Diwani wa Kata hiyo, Hedson William amewataka wakazi wa Mwaya kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu ambapo ujenzi wa daraja la muda ukiendelea.

Diwani huyo amesema kuwa ujenzi wa daraja la muda ni nguvu za wananchi, Mbunge pamoja na wadau mbalimbali ili kutatua changamoto inayo wakabili wakazi wa Kata hiyo wakati Wakala wa Barabara (TANROADS) wakiendelea na utaratibu wa kujenga daraja jipya la mto Ruaha.

“Nitoe rai kwa wakazi wa Mwaya wawevumilivu katika kipind hichi, nilizungumza na Tanroads wakasema wapo njiani kuja eneo la tukio na leo kazi ya ujenzi wa daraja utaanza” William amewahakikishia wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa daraja la muda, Emmanuel Machael amesema ujenzi wa daraja hilo la muda ukatamilika kwa haraka ili kuwezesh watu wataanza kupita pamoja na vyombo vya moto ikiwemo pikipiki.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments