Yanga kileleni!

DAR ES SALAAM: USHINDI wa bao 1-0 dakika 85’ umeifanya Yanga SC kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa points 34 katika michezo 13.

Licha ya mlinda lango wa Dodoma Jiji FC, Mohamed Hussein kuchomoa michomo 6 iliyolenga lango lakini shuti mpenyezo la Mudathir Yahya Abbas akiunganisha pasi ya Nickson Kibabage ilimshinda nyanda huyo.

Kama ambavyo nyakati za furaha hazidumu, nyakati za huzuni pia hazidumu. Walima zabibu walikuwa wafanisi zaidi katika kulinda lango lao na kuufanya Uwanja wa Azam complex kujawa na majonzi kwa kitambo kadhaa.

Matokeo haya yanawafanya Dodoma Jiji FC kusalia katika nafasi ya saba ya msimamo wa Ligi Kuu, wakivuna points 18 katika mechi 14.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Azam FC baada ya kukusanya points 31 katika michezo 13. Nafasi ya tatu yupo mnyama Simba FC aliyevuna points 26 katika michezo 11.

Timu zilizopo mkiani ni Ihefu SC, nafasi ya 14, michezo 14 points 13. Mashujaa FC nafasi ya 15, michezo 13 alama 9 huku Mtibwa Sugar FC wakiburuza mkia katika nafasi ya 16, points 8 katika michezo 13.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments