MOROGORO: Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mwa Ligi kuu Tanzania bara baada ya kuitandika KMC 3-0 kwenye mchezo uliomalizika muda mchache uliopita Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha alama 43 katika michezo 16 walioshuka dimbani msimu huu na kuongeza wigo wa tofauti ya alama baina yake na Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na alama 36.
Magoli ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na kiungo Mudathir Yahya aliyeingia kambani mara mbili dakika ya 01 ,54 na Pacome Zouzoua aliyepigilia msumari wa tatu na wa mwisho dakika ya 59 ya mchezo.
0 Comments