Al Ahly waingia 18 za Simba

 WAPINZANI wa Simba SC katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Al Ahly SC imewasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu nchini Misri na CAFCL wamepost video inayoonesha wakiwasili huku ikichagizwa na maneno “Habari, Tanzania 👋🇹🇿”.

Mnyama Simba atakabiliana na mashetani hao wekundu mnamo Machi 29 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Aprili 05 nchini Misri saa 5:00 usiku.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments