Heka heka za kampeni zilizodumu kwa takribani zaidi ya siku 14 kwa ajili ya kuwania nafasi ya Udiwani katika Kata Msangani Jimbo la Kibaha mjini zimetamatika hii leo kwa kishindo cha aina yake huku chama cha CCM kikitamba kushinda kwa kishindo.
Kampeni hizo ambazo zimefungwa rasmi na Mwenyekiti wa jumuiya wa wazazi ya chama chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Jakson Kituta na kuhudhuliwa na wananchi,wanachama pamoja na viongozi wa CCM wa ngazi mbali.mbali.
Akifunga kampeni hizo Mwe nyekiti huyo aliwahasa wananchi wa kata ya Msangani kuhakikisha kwamba wanamchagua kwa kishindo mgombea wa CCM ili aweze kuwaletea maendeleo.
Alisema kwamba ana imani kubwa na mgombea huyo endapo akichaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Msangani ataweza kushirikiana bega kwa bega katika kuweka mipango madhubuti ya kimaendeleo.
"Nawaomba wananchi wa kata hii ya Msangani msifanye makosa kabisa hata kidogo kikubwa nimekuja hapa ili kuweza kumnadi mgombea wetu kwa hiyo kitu kikubwa mjitokeze kwa wingi kumpigia kura na tutashinda kwa kishindo ,"alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mji Mwalimu Mwajuma Nyamka alisema lengo la CCM ni kutekeleza ilani ya Chama hivyo wananchi wamchague mgombea wao ambaye ataweza kusikiliza kero na changamoto za wananchi.
Nyamka alibainisha kwamba mgombea wao ana sifa zote hivyo wananchi wa kata ya Msangani wanapaswa kumpa kura nyingi mgombea wa CCM ili aweze kushinda kwa kishindo na kuwaletea mabadiliko.
"Hapa leo tumekuja kumnadi mgombea wetu na kitu kingine mambo ya utekelezaji wa Ilani ya chama tulishaisema katika uchaguzi uliopita kwa hivyo hapa tumekuza kukazia tu mambo tuliyoyafanya katika miradi ya maendeleo,"alisema Mwalimu Nyamka.
Kwa upande wake mgombea udiwani katika kata hiyo ya Msangani Yohana Gunze alikishukuru kwa dhati chama chake cha CCM kwa kuweza kumuamini kugombea katika nafasi hiyo.
Gunze alisema kwamba endapo atashinda katika nafasi hiyo atowaangusha kabisa wananchi na badala yake atashirikiana nso kwa hali na mali katika masuala mbali mbali ya kiuchumi na kimaendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mjini Mussa Ndomba alibainisha kwamba katika kata hiyo ilani ya chama imetekelezeka kwa kiwango kikubwa katika sekta mbali mbali ikiwemo afya,elimu,maji mindimbinu ya barabara na mambo mengine.
Nao badhi ya madiwani kutoka kata mbali mbali waliohudhulia katika ufungaji wa kampeni hiyo walimnadi mgombea huyo na kumuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha pindi atakaposhinda.
Naye Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Issack Kalleiya aliwataka wanachama na wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura huku akiwataka siku hiyo ya uchaguzi wasivae sare yoyote ya chama.
Uchaguzi wa kujaza nafasi ya udiwani katika kata ya Msangani na maeneo mengine ya Jimbo la Kibiti pamoja Jimbo la Bagamoyo unatarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.
0 Comments