Katibu wa NEC , Idara ya Organaizesheni Ndugu. Issa Haji Ussi (Gavu) tayari amewasili katika Ukumbi wa Mkuki House na kupokelewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndugu. Mary Chatanda (MCC).
Ndugu. Gavu amefika na kuungana na UWT katika Kongamano la Kumshukuru na Kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya utekeleza wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025 kwa kipindi cha miaka 3 akiwa madarakani kuanzia 2021 - 2024.
Katika ushiriki wake, Ndugu. Gavu ndiye Mgeni rasmi akimwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu. Balozi. Emmanuel Nchimbi.
0 Comments