Dkt Jakaya Kikwete Apongeza Kasi Ya Ukuaji Taasisi Za Fedha, Aipongeza NBC Ushirikiano Na Wateja.

 

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ukuaji pamoja na uimara wa taasisi za fedha hapa nchini huku akizisisitiza taasisi hizo kuendelea kujiendesha kwa weledi zaidi ili ziweze kuongeza tija katika kuchochea ongezeko la uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo biashara.


Akizungumza kwenye hafla fupi ya futari iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Dkt Kikwete aliitumia benki ya NBC kama mfano muhimu katika kuthibitisha uimara wa taasisi hizo ambazo pamoja na kuongeza viwango vya mikopo na huduma mbalimbali kwa wateja pia zimeweza kutengeneza faida kubwa na hivyo kuendelea kijiimarisha zaidi.

“Napotoa pongezi na shukrani naamanisha kwa dhati kabisa kwasababu mabadiliko (reforms) mengi ya taasisi ya kifedha yalifanyika mimi nikiwa Waziri wa Fedha kwa wakati ule hivyo najua vema tulipo sasa na tulipotoka. Leo hii nikiona mabenki yanatangaza faida kwa mabilioni ya fedha yananithibitisha wazi kabisa kuwa zile ‘reforms’ tulizozifanya kipindi kile zimefanikiwa,’’ alibainisha Dkt Kikwete huku akiitolea mfano benki ya NBC iliyotengenza faida ya sh bilioni 122 kwa mwaka uliopita.

Akitumia mifano na historia zaidi, Dkt Kikwete alitumia muda mwingi kuelezea namna wateja walivyopitia wakati mgumu kupata huduma za kifedha kwenye taasisi hizo kabla ya serikali kuingilia kati na kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kufunga na kubadili muundo wa uendeshaji na umiliki kwa baadhi ya benki hizo.

‘’Leo hii changamoto zote zimebaki historia. Fedha kwenye Uchumi ndio damu ya Uchumi. Sekta ya fedha ikiteteleka ndio chanzo cha uchumi kuporomoka. Uchumi wa nchi unategemea sekta ya fedha hivyo ikiteteleka kila kitu kinaharibika. Hivyo nawapongeza sana NBC na taasisi nyingine zote kwa kuendelea kutoa huduma zenu kwa weledi huku pia mkiendelea kujiimarisha kimitaji,’’ aliongeza.

Akizungumzia matukio ya benki hiyo ya kuandaa futari kwa ajili ya wateja wake kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini Dkt Kikwete alisema matukio kama haya yanaongeza imani kwa wateja wa benki hiyo kwa kuwa ni moja ya thibitisho kuwa uhusiano wa benki na mteja haushii kwenye biashara pekee bali pia unagusa imani za wateja.

“Matukio ya futari kama haya yanasababisha wateja wenu tunajisikia vizuri kwa kuwa tunaona kwamba tunahudumiwa na benki ambayo pia inajali maslahi yetu kiimani’’ aliongeza.

Awali akizungumzia hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi, alisema ni muendelezo wa utaratibu wa benki hiyo kwa miaka 15 sasa ikilenga kujumuika na wateja wake kama hatua ya kuonyesha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema benki hiyo inaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba wake kupitia mfungo na kufanya maombi.

“Huu ni mwezi ambao pia unatukumbusha kufanya kilicho chema mbele za Mungu wetu. Kwa kuwa NBC siku zote tupo karibu imani za wateja wetu tumeamua kuandaa futari hii ili kujumuika na wenzetu kufanikisha hilo.” Alisema Sabi.

Zaidi Sabi aliangazia huduma maalum ya benki hiyo, "La Riba," iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wenye imani ya kiislamu kwa kuzingatia kanuni za dini hiyo katika masuala yanayohusiana na fedha na mtazamo wa dini hiyo kuhusiana na riba.

‘’NBC ndio benki ya kwanza kubwa kuanzisha huduma za kibenki zinazozfuata misingi ya kisheria kupitia La Riba Banking ikiwemo akaunti za akiba na biashara kwa watu binafsi, wajasiriamali na makampuni makubwa. Benki pia inayo akaunti ya muda maalum (fixed deposit) inayofuata misingi ya sharia yaani ‘Mudharaba’. Zaidi kupitia dirisha hilo la La Riba tunatoa huduma ya mikopo kwa wafanyanyabiashara wakubwa na wa kati, wajasiriamali wadogo na wafanyakazi wa sekta ya umma na sekta binafsi,’’ alibainisha Sabi.

Hafla hiyo ya futari ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Kulia) wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam jana. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.


Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.



Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.



Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC pamoja na wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini humo . Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini humo. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments