DKT. NCHEMBA ATETA NA WAZIRI WA UJENZI

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta ya ujenzi ili sekta hiyo iweze kuongeza mchango wake katika Uchumi na maendeleo ya watu. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.


Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), akieleza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wakati alipoongoza ujumbe wa Wizara yake walipokutana na ujumbe wa Wizara ya Fedha ukiongozwa na Waziri wake Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwa ajili ya kujaili maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – maamry Mwamba, akifafanua jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), walipojadili maendeleo ya sekta ya ujenzi kupitia Wizara hiyo. Mkutano huo uliwashirikisha pia Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Mhandisi Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mhe. Balozi Mhandisi Aisha Amour na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara hizo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akisikiliza maelezo ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Mhandisi Godfrey Kasekenya (Mb), wakati wa mkutano kati ya Waziri huyo na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour na wajumbe wengine wakiteta jambo, baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Mawaziri hao uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – maamry Mwamba (wa pili kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhe. Balozi Mhandisi Aisha Amour, wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Mawaziri hao ulioangazia maendeleo ya Wizara ya Ujenzi, uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El – maamry Mwamba na Kamishna wa Bajeti, Bw. Meshack Anyingisye, wakifurahia jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) (hawapo pichani), katika ukumbi wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) (wa kwanza kushoto), wakiwa na kikao kilichowashirikisha wajumbe kutoka pande hizo mbili kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Fedha)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments