Wananchi wa kijiji cha Msomera wametuma salamu za pongezi kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi ikiofanyika katika kuwezesha upatikanaji wa huduma muhimu ya Majisafi na Salama pamoja na Maji kwaajili ya mifugo na pia kuridhishwa na kazi nzuri ya usimamizi wa Wizara ya Maji chini ya Mhe. Jumaa Aweso jambo lililopelekea shangwe kubwa na kumbeba juu na kumtuma afikishe shukrani zao za dhati kwa Mheshimiwa Rais.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso (Mb) amefanya ukaguzi wa miradi ya maji katika Kijiji cha Msomera,Wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga kuona hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi, ikiwemo miradi ya uchimbaji wa mabwawa makubwa ya maji.
Aidha, Aweso amesema tayari Serikali kupitia Wizara ya Maji imechimba visima 21 vyenye thamani ya shilingi milioni 480, uchimbaji wa bwawa kubwa la maji la Msomera lenye thamani ya shilingi bilioni 1.9,ambalo ujenzi wake umefika asilimia 75, na miradi hii inanufaisha wananchi zaidi ya elfu 13 wa katika kijiji cha Msomera na mifugo zaidi ya milioni Moja tangu wananchi wa Ngorongoro walipoamua kuhamia kwa hiyari kijijini Msomera mwaka 2022
Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amesema Wizara ya Maji inakusudia kuzungumza na Wizara nyingine mtambuka kwa lengo la kujenga Bwawa kubwa la maji la kimkakati katika Kijiji cha Msomera kwa lengo likiwa kuwahudumia wananchi na mifugo.
0 Comments