JAMUKAYA RAMADHAN CUP 2024 KUTIMUA VUMBI UWANJA WA SHY COM, TIMU 16 KUWANIA UBINGWA

 

Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akizungumza na Vyombo vya Habari leo Jumatano Machi 6,2024
Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, Wakili John Palamagamba Kabudi akizungumza na Vyombo vya Habari leo Jumatano Machi 6,2024

Michuano ya Jamukaya Ramadhan Cup msimu wa 2024 inatarajia kuanza kutimua vumbi ukatika uwanja wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom) Mjini Shinyanga kwa timu 16 kuwania ubingwa wa michuano hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatano Machi 6,2024 Meneja Rasilimali Watu, Utawala na Sheria wa Kampuni ya Jambo Group, amesema Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe Machi 14, 2024 hadi Aprili 3,2024.

Ameeleza kuwa michezo itakuwa inafanyika kuanzia saa 3:00 usiku na kwamba lengo la mashindano hayo ni kusaidia watu wenye uhitaji wakiwemo wajane na watoto yatima.

"Ligi hii ya Jamukaya Radhaman Cup itafanyika katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na itakuwa ligi ya mtoano dhumuni kubwa ni kusaidia watoto yatima na wajane. Maandalizi ya kufunga taa uwanjani yanaendelea. Mwisho wa kuchukua fomu za kushiriki michuano hii ni Machi 11,2024 ambapo siku hiyo pia tutatangaza zawadi zitakazotolewa kwa washindi katika kinyang'anyiro hicho",amesema Wakili John.

Wakili John amebainisha kuwa, upatikanaji wa timu zitakazoshiriki ni kupitia usajili unaoendelea kufanyika katika ofisi za Jambo FM (Ibadakuli) kwa timu mbalimbali za mitaani na taasisi kwa gharama ya shilingi 250,000/= na kujipatia seti ya jezi bure.

Amesema ulinzi na usalama wa mashindano hayo yatayokuwa yanafanyika usiku upo wa kutosha hivyo kuwaomba mashabiki wa soka na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi ambapo kiingilio ni shilingi 500 na kila shabiki atapatiwa kinywaji cha bure kwa kila mchezo.
Chanzo Na Malunde

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments