MADEREVA WA MABUS YAENDAYO MIKOANI WAPATIWA HUDUMA YA UPIMAJI MACHO

Hii ni wiki ya maadhimisho ya Ugonjwa wa Shinikizo la macho au Presha ya Macho duniani ambapo hospitali ya CCBRT,kwa kushirikiana na hospitali ya Barrack PolisI Kilwa Road na halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, wameadhimisha kwa kutoa huduma ya upimaji macho kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani kwa lengo la kunusuru uoni wa macho yao kutokana na kazi muhimu wanayoifanya.

Pia huduma hii inatolewa kwa mtu yoyote anayefika kituoni hapo ambapo tangu kuanza kwa zoezi hilo la wiki moja tarehe 12.3.2024 zaidi ya watu 400 walikuwa wamepatiwa huduma.

Ugonjwa wa presha ya macho unatajwa na wataalamu wa afya ya macho duniani kuwa wa kwanza kusababisha upofu usiotibika duniani.

Daktari wa Macho Dk. Erick Raphael (aliyesimama) kutoka hospitali ya Polisi Barrack Kilwa Road akimhudumia mmoja wa wananchi waliofika kupata huduma katika kituo kikuu cha Mabasi Magufuli Mbezi Luis, Dar es Salaam.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments