Majaliwa: Ni suala la Muda Tu Ujenzi Wa Reli ya Kati

 Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa amesema mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati mpaka sasa umeshafika maeneo yote yanayopaswa kufikiwa.

Majaliwa amesema hayo leo Machi 27, 2024 akihitimisha kampeni ya Kurasa 365 za mama katika ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.

Amesema, ‘tuna mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati ambao umeshafika kwenye maeneo yote ambayo reli hiyo inatakiwa kufika, ujenzi wa reli kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro umekamilika na umeshafanyiwa majaribio mara mbili,”.

Amesema, ujenzi wa reli kutoka Morogoro mpaka Makutopora nao umekamilika kwa kiasi cha zaidi ya asilimia 96 maeneno yaliyobaki ni maboresho na viunganishi kuhakikisha kila kitu kimekamilika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments