Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi zawadi Rais ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Utalii Duniani (World Travel and Tourism Council-WTTC) Julia Simpson mara baada ya kikao cha kujadili namna ya kushirikiana kutangaza utalii, kilichofanyika katika banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Utalii ya ITB jijini Berlin, Ujerumani leo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na makampuni makubwa ya utalii ya nchini Ujerumani yenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania katika kikao kilichofanyika kwenye banda la Tanzania katika Maonesho ya Utalii ya ITB jijini Berlin, Ujerumani leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi wa Sayansi, Makumbusho ya Viumbe hai Berlin, Dkt. Andreas Kunkel (kushoto) akifafanua kuhusu mabaki ya samaki yaliyohifadhiwa katika jumba la Makumbusho hayo nchini Ujerumani. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utali, Dkt. Thereza Mugobi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi wa Sayansi, Makumbusho ya Viumbe hai Berlin, Dkt. Andreas Kunkel (kushoto) akifafanua kuhusu mabaki ya mjusi mkubwa duniani aina ya “Dinosaur”yaliyohifadhiwa katika jumba la Makumbusho hayo nchini Ujerumani.
Badhi ya Mafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake wakihudumia wageni katika banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Utalii ya ITB Berlin nchini Ujerumani.
0 Comments