Majaliwa ametoa maagizo hayo mapema Leo hii Jijini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali wa Tanzania uliobeba kauli mbiu inayosema "UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA KISHERIA KWA WANANCHI NI NGUZO MUHIMU KWA USTAWI WA JAMII".
"Nitumie nafasi muhimu kabisa na kwa msisitizo,Maafisa Sheria pamoja na Mawakili wa Serikali wote tekelezeni majukumu yenu ya kisheria kwa Weledi, Uadilifu, Uaminifu,Uajibikaji,Usiri, Umakini na kwa kujituma".
Sambamba na hayo pia Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa Chama hicho washirikiane na Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria zinatolewa kwa wananchi wote wenye uhitaji wa huduma za kisheria bila ubaguzi wa namna yetote ile.
"Uongozi wa Chama cha Mawakili wa Serikali shirikianeni na Wizara ya katiba na Sheria,vilevile na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria unatolewa kwa wanachi wote wenye uhitaji bila ubaguzi wa namna yetote".
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt Pindi Chana ametoa Rai yake kwa wana Sheria wenzake kuwa ni wajibu wao kuhakikisha kwamba wanawasikiliza wa Tanzania,kama jinsi kauli mbiu inavyoelekeza kuhusu upatikanaji wa huduma za kisheria kwa wananchi na kama viapo vya kisheria vinavyoelekza.
"Nitoe rai kwa wanasheria wenzangu ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba tunawasikiliza wa Tanzania,na kama jinsi ambavyo kauli mbiu yetu ilivyo upatikanaji wa huduma za kisheria kwa wananchi ni nguzo muhimu kwa ustawi wa jamii,hivyo ni jukumu letu la msingi kuwasikikiza wananchi,kuwaelekeza,kuwashuri kama jinsi ambavyo viapo vyetu vya Sheria vilivyo".
Naye Raisi wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania Michael Luena pamoja na kuelezea mafanikio na changamoto zilizopo ndani ya chama cha Mawakili ya kukosa Ofisi za kudumu na kukosa fedha kwaajili ya uendeshaji wa shughuli za chama pia ametoa ahadi mbele ya Waziri Mkuu kuwa watatekeleza majukuyao kwa Haki na Weledi.
"Mawakili wa Chama cha Mawakili wa Serikali tunapenda kuahidi kuwa tutaendelea kutekeleza majukumu yetu kwa haki,weledi na kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za Serikali ili kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu yetu isemayo upatikanaji wa huduma za kisheria kwa wananchi ni nguzo muhimu kwa ustawi wa jamii".
Mkutano huo uliofanyika Leo Jijini Dodoma ni mkutano wa pili tangu kuanzishwa kwa chama hicho cha Mawakili wa Serikali wa Tanzania ambapo rasmi ulizunduliwa 29/09/2022 na Raisi wa Jamhuri ya Mungano wa Mh Dkt Samia Suluhu Hassan.
0 Comments