MGODI WA BARRICK BULYANHULU WAONGEZEWA MUDA WA LESENI YA UCHIMBAJI

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba (kushoto) akimkabidhi leseni ya kuongezewa muda wa uchimbaji wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido katika hafla hiyo , wanaoshuhudia nyuma (kushoto) ni Waziri wa Madini, Mh.Antony Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha. Leseni hii mpya iliyotolewa ni ya kipindi cha miaka 27.
---
Serikali kupitia Wizara ya Madini imeongeza muda wa leseni ya uchimbaji wa dhahabu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, uliopo katika wilaya za Kahama na Nyang’hwale mkoani Shinyanga kwa kipindi cha miaka 27 kuanzia mwaka huu.

Hafla ya kukabidhi leseni hiyo ilifanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Maofisa waandamizi kutoka Wizara ya madini, Wakuu wa mikoa ya Tanga na Shinyanga na wadau mbalimbali kutoka sekta ya madini ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri wa Madini, Mh.Antony Mavunde.
Aliyekabidhi leseni hiyo ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, na Mwakilishi wa Barrick, aliyepokea leseni hiyo kwa niaba ya kampuni ni Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido.

Mgodi wa Bulyanhulu tangu uanze kuendeshwa na kampuni ya Barrick kwa kushirikiana na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals, umefanikisha kuleta mafanikio chanya katika kukuza uchumi wa nchi ,kuongeza fursa za ajira sambamba na kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii kupitia fedha za uwajibikaji wa jamii (CSR) ambayo inazidi kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yanayozunguka mgodi huo hususani katika sekta ya afya na elimu.
Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido (kushoto) katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa makampuni ya uchimbaji wa madini waliokabidhiwa leseni katika hafla hiyo.

Maofisa Waandamizi wa Barrick waliohudhuria hafla hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu.

Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini, Antony Mavunde katika hafla hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments