''ALIEONDOKA KULWA ALIEKUJA DOTO MKUU WA MKOA SINGIDA'' RC.HALIMA DENDEGO


                                       
MKUU wa Mkoa wa Singida Bi Halima Dendego ameripoti Leo kwenye kituo chake kipya cha kazi na  amesema kuwa aliyeondoka kulwa na aliyekuja doto me sina neno changamoto tufanye kazi kwa pamoja ili tupate majibu.

Bi.Halima Dendego amesema hayo wakati akabidhiwa ofisi na aliekuwa mkuu wa mkoa Singida Peter Serukamba.

“Katika kilimo tunakwenda kuleta tija katika mazao ya kimkakati  yaweze kuwa mkombozi kwa mkulima kwa kuendeleza pale alipo kuwa anafanya kaka yangu Peter Serukamba  lakini kuongeza kiwango Cha mapato “amesema Mkuu wa mkoa huyo.

Pia Bi.Halima  amevitaja vipaumbele vingine ni miradi ya kimkakati na ubunifu wa fursa zinazotokana na miradi hiyo, ulinzi na usalama wa watu na mali zao, udhibiti wa mfumko wa bei hasa kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma na Ramadhani.

Kwa Upande Wa Mwenezi Wa CCM Mkoa Wa Singida Bw. Eliphas Lwanji amesema kuwa mabadiliko ya uongozi yanayofanywa na Rais Samia yamelenga katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kiutendaji .

Nae Meya Wa Singida Manispaa Bi Yagi Kiaratu  amesema kuwa wao kama vingozi wa Halmashauri  wamejipanga katika kusimamia malengo makuu manne ambayo ni kusimamia miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato,kusikiliza na kutatua kero za wananchi lakini na ubunifu katika kuzifikia fursa za kiuchumi zilizopo kwenye wilaya zao.

                                        






 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments