RIYADH, Saudi Arabia: CRISTIANO Ronaldo amefungiwa mechi moja kwa kosa la kufanya kitendo kinachodaiwa kuwa cha kuudhi wakati wa mchezo wa ligi ya Saudi Arabia kati ya Al Nassr na Al-Shabab.
Baada ya Al-Nassr kushinda 3-2 Jumapili, picha za video zilimuonesha Ronaldo akionesha ishara ya kuwasikiliza mashabiki na kuchezesha mkono wake karibia na nyonga, ishara iliyoonekana kuwalenga mashabiki wa Al-Shabab.
Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Shirikisho la Soka la Saudi Arabia (SAFF) ilitangaza adhabu hiyo kwenye mitandao ya kijamii leo Alhamisi.
Mechi inayofuata ya ligi ya Al-Nassr itakuwa nyumbani dhidi ya Al-Hazm leo.
Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United pia atalazimika kulipa faini ya Saudi Riyal 20,000 ($5,333) kwa Al-Shabab, ili kulipia gharama za klabu hiyo kuwasilisha malalamiko hayo, na nusu ya kiasi hicho kwa shirikisho hilo.
0 Comments