SERIKALI INATAKIWA KUSHIRIKIA NA WADAU WA SECTA BINAFSI ILIKUWALETEA MAENDELEA WANANCHI

Kampuni ya Kijiji cha Nyuki iliyopo mkoani Singida imetoa wito kwa Viongozi wa Serikali na Chama Tawala kushirikiana na Wadau wa Sekta Binafsi kuhakikisha wanakuwa na mtazamo mmoja wa kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Singida na nchi kwa ujumla.
  Mkurugenzi wa kijiji cha Nyuki PHILEMON KIEMI alitoa wito huo wakati akizungumza na waadishi wa habari, baada ya kupokea ugeni kutoka ubalozi wa Canada waliokuja kutembelea Kijiji cha Nyuki.
                                   
Alisema kijiji cha Nyuki kinakishukuru chama Tawala na serikali iliyopo madarakani kwa jitihada inazozifanya kuwaletea wananchi maendeleo.

KIEMI alisema wao kama Kijiji cha Nyuki wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha KIEMI alitoa wito kwa wataalam wa Ardhi wa wilaya za Mkoa wa Singida watenge maeneo ya kufugia Nyuki tofauti na shughuli nyingine za kibinadamu ambazo zinaathiri ufugaji wa Nyuki.
                                    
Alisema endapo maeneo hayo ya ufugaji nyuki yatatengwa tofauti na maeneo mengine ya shughuli za kibinadamu kama vile kilimo na Mifugo itasaidia kutatua migogoro ya ardhi isiyo ya lazima.

Hata hivyo KIEMI alitoa wito kwa jamii kuondoa tofauti zilizopo za Kisiasa, Kidini na Kiuchumi na badala yake waje na fikra na mitazamo maendeleo katika Jamii.

Kijiji cha Nyuki pia kimewekeza Kiwanda cha kuchakata Asali ambacho kitawasaidia wananchi wa Mkoa wa Singida kuipa Thamani Asali yao ili iweze kuingia kwenye masoko ya kimataifa.
                                        
KIEMI alisema Kiwanda hicho kitasaidia kuongeza uzalishaji wa Asali kutoka Tani 450 hadi kufikia Tani 1000 kwa Mwaka.
 
Chanzo Zaraafricablog.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments