MSHAMBULIAJI wa Azam Fc na raia wa Zimbabwe Price Dube rasmi amewaaga mashabiki wa timu yake kwa kuandika ujumbe katika mitandao ya kijamii na kuwashukuru mashabiki hao kwa mchango mkubwa ambao wameutoa.
Hivi karibuni kulitokea mvutano baina ya mchezaji huyo na timu yake kutaka kuvunja mkataba na kuangalia maisha mengine nje ya klabu hiyo lakini timu hiyo ilitaka afuate utaratibu wa mkataba aidha kulipa gharama ya kuvunja mkataba kwa gharama ya dola laki tatu au asubiri mkataba wake uishe 2027.
Dube hajacheza mechi kadhaa za ligi kutokana na majeruhi aliyoyapata hivi karibuni
0 Comments