Waandishi wa habari wafa kwenye ajali

LINDI; WAANDISHI wa habari wawili mkoani Lindi wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Nyamwage mkoani Pwani wakiwa njiani kurejea Lindi wakitokea jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolea na Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Lindi, Fatuma Maumba, imesema ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia leo Machi 26, 2024 na waliofariki ni Josephine Kiberiti wa Sahara Media Group na Abdallah Nanda wa Channel Ten.

“Tunachokifanya kwa sasa ni kushughulikia miili ya wenzetu ifike hapa mkoani Lindi kwanza na baada ya hapo tutaweka utaratibu wa kuwaaga wenzetu, ” imesema taarifa hiyo ambayo haikufafanua kwa undani kuhusu ajali hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments