Watu 11 Wakamatwa Kisa Kula Mchana

POLISI wa Kiislamu wanaofahamika kwa jina la Hisbah Kaskazini mwa Jimbo la Kano nchini Nigeria wamewakamata waislamu 11 kwa kula mchana ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Msemaji wa Hisbah, Lawal Fagge aliripoti kukamatwa kwa wanaume 10 na mwanamke.

“Tulipokea watu 11 siku ya Jumanne akiwemo mwanamke aliyekuwa akiuza njugu ambaye alionekana akila kutoka bidhaa zake, na baadhi ya watu walituarifu,” Fagge alisema.

“Wengine 10 walikuwa wanaume na walikamatwa katika jiji lote hasa karibu na masoko ambapo shughuli nyingi hufanyika.”

Washtakiwa 11 baadaye walifutiwa makosa yao baada ya kuapa kutokula au kunywa. Zaidi ya hayo, familia zao ziliombwa kuhakikisha wanafunga.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments