Bajaji za Umeme Nchini Kushuka Bei

KITUO cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesaini mikataba miwili ya makubaliano ya uwekezaji baina ya Kampuni ya Mass ya nchini India na Kampuni ya Utegi Technical Interorises international limited ya Tanzania.

Mkataba wa kwanza umesainiwa kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha kuunganisha Bajaji zinazotumia nishati ya umeme, na wa pili unalenga kuendeleza kampeni ya kutangaza fursa za uwekezaji nchini.

Wakisaini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TIC, Gilliard Terry amesema mkataba wa pili unahusisha kituo hicho na kampuni ya Mass ya nchini India.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampuni ya Utegi Technical Interprises Limited International inayojishughulisha na uwakala wa forodha na usafirishaji, Otieno Igogo amesema watawekeza dola milioni saba kwa ajili ya kuunganisha hizo bajaji ndani ya miezi sita kuanzia sasa.

Matokeo ya Mkataba huo ni kutokana na ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini India ambapo baadhi ya wafanyabiashara waliongozana na Rais walitumia mwanya huo kupata wabia wa kibiashara.

Bei ya bajaji hizo zitakazounganishwa zitashushwa hadi kufikia sh milion nane kutoka milioni 10 hadi 13, ambazo zitatoa fursa ya ajira.

Katika uzalishaji wa mwanzo utawezesha kiwanda kuingiza bajaji 100 sokoni.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments