MIFUGO MBARONI NA WATUHUMIWA KUTOROSHA MIFUGO NJE YA NCHI.

 Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakitorosha mifugo 514 Kwenda Nchi Jirani huku wakitumia vibali vya kampuni isiyohusika na Mifugo hiyo.

Akitoa taarifa hiyo kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo nchini kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua amesema Kikosi hicho kwa kushirikina na wananchi Aprili 06,2024 Katika Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha waliwakama watu wawili wakiwa na mifugo 514 ambayo walikuwa wakiitorosha Kwenda nchi Jirani.

Kamanda Pasua amebainsha kuwa watuhumiwa hao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na utoroshaji na kukiuka taratibu za uuzaji wa Mifugo hapa Nchini.

SACP Pasua amesisitiza na kuwataka wananchi kufuata taratibu za uuzaji wa mifugo ili kutokukumbana na mkono wa sheria na kulikosesha mapato Taifa huku akisema Jeshi hilo litaendelea kuwakamata wale wote watakao kiuka taratibu.

Nao baadhi ya wafanya biashara wa mnada huo wa mpakani Namanga wamewaomba wananchi wenzao kufuata taratibu zilizopo ili kutokukumbana na mkono wa sheria pindi wanapotaka kusafirisha mifugo yao nje ya nchi.

Daktari wa Mifugo Mnada wa Mpakani Namanga Longido Mkoani Arusha amewataka wafanya biashara kufuata taratibu huku akiwaomba wafanya biashara hao kufika na vibali vilivyo kamilika ili kuondoa usumbufu na wasimamizi wa Mnada huo.








TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments