WAKINA MAMA WAMETAKIWA KUJIFUNGULIA KWENYE VITUO VYA AFYA.

Mwenyekiti wa Jumiya ya Wazazi Mkoa wa Singida BERTHA NAKOMOLWA amewataka akina Mama wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya afya ili kupunguza vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.


NAKOMOLWA alisema hayo wilayani Mkalama katika Ziara ya Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo, ikikagua Kituo cha Afya cha Kata ya GUMANGA, ambacho kimeanza kutoa huduma za Afya kwa wananchi wa Kata hiyo.

Alisema, hakuna haja ya akina Mama kujifungulia nyumbani wakati kituo cha afya kipo na kina Vifaa na wahudumu wazuri.

NAKOMOLWA aliongeza kuwa kujifungulia nyumbani ni hatarii kwa Mama na Mtoto hasa pale itakapotokea changamoto, hali inayoweza kusababisha vifo kwa Mama na Mtoto.

Aidha alisema endapo akina Mama watatumia vituo vya afya vilivyo maeneo yao, itasaidia kupunguza vifo hivyo vya Mama na Mtoto.

Hata hivyo Jumuiya hiyo ya Wazazi Mkoa wa Singida imeishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kwa kujenga ktituo cha Afya Kata ya GUMANGA Wilayani Mkalama, ambacho kimesaidia kuondoa changamoto ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata hudumu za Afya.

Wajumbe wa Kamati hiyo walisema serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga kituo, hivyo wanaishukuru kwa kusogeza huduma za karibu na wananchi.

Kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Singida imeendelea na ziara yake ya kutembelea na kukagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia Ilani ya CCM na kufanya mikutano ya hadhara na Wananchi, katika Wilaya zote za Mkoa wa Singida.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments