WANANCHI ITIGI WAMSHUKURU RAIS , KITUO CHA AFYA KUANZA UPASUAJI

 


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida, Hussein Simba, akizungumza wakati akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Aprili 3, 2024. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ayubu Kambi na na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jonathan Hemed.

..................................

Na Mwandishi Wetu, Itigi

WANANCHI wa Kata ya Rungwa iliyopo wilayani Itigi mkoani Singida wamemshuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea Kituo cha Afya ambapo sasa wajawazito wameanza kupata huduma ya upasuaji na kuondokana na changamoto waliokuwa nayo ya kufuata huduma hiyo Hospitali ya St. Gasper iliyopo Itigi.

Diwani wa Kata hiyo Said Sudi akitoa shukurani hizo kwa niaba ya wananchi wake wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichoketi Aprili 3, 2024 alisema hawana cha kumlipa Rais Samia zaidi ya kumpa kura zote katika uchanguzi mkuuu utakaofanyika mwakani.

"Kata yetu tutampa kura asilimia 100 mama yetu kwa kazi kubwa aliyotufanyia si kwa kituo cha afya pekee bali na miradi mingine mingi iliyotekelezwa. wajawazito walikuwa wakilazimika kusafiri umbali wa kilometa 194 pale walipohitaji kupata huduma ya upasuaji lakini sasa wanaipata hapahapa nyumbani ni jambo la kumshuruku sana Mungu kupitia Rais wetu," alisema Sudi.

Sudi alisema Rais Samia aliwapa Sh. Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya ambacho kimeanza kutoa huduma hiyo Februari 27, 2024 ambapo wajawazito watano wamenufaika na huduma.

Alisema wajawazito walionufaika na huduma hiyo ni kutoka vitongoji vya Mkora A na B na kata za jirani za Kiloli na Kambikatoto.

Sudi alitumia nafasi hiyo kuomba wasaidiwe kupata gari la kubebea wagonjwa, mashine ya kufulia na kunyoshea nguo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Hussein Simba alisema ukusanyaji wa mapato katika halmashauri hiyo upo vizuri hadi kufikia mwezi februari walikuwa wamefikia asilimia 95 ya mapato ya Serikali mapato huru na mapato lindwa ilikuwa ni asilimia 35 na kuwa wanaamini kwa kasi hiyo hadi mwezi machi ambao bado hawajaujadili watafikia asilimia 100.

Simba alisema kupitia fedha za Serikali kuu na wahisani wamefikia asilimia 77 ya lengo ambapo zaidi ya Sh.Bilioni 4.9 halmashauri hiyo imekwishapewa ili kukamilisha miradi mbalimbali na kuwa asilimia iliyobaki ni ndogo ambapo amewahimiza madiwani kuisimamia miradi hiyo kwa kufanya kazi kwa vitendo zaidi badala ya maneno ili kufikia malengo ya wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota, aliomba miradi yote inayotekelezwa ikikamilike ifikapo Aprili 30, 2024 ambapo pia aliwaomba madiwani kuhimiza kampeni ya kupata madawati kufuatia kuwepo kwa changamoto ya kukosekana kwa madawati katika shule zote wilayani humo.

Aidha, Lwota alihimiza mazao yote kuuzwa kwa njia ya stakabadhi gharani badala ya kuuzwa kiholela jambo linalosababisha Serikali kukosa mapato ambapo utaratibu wa kuyauza mazo hayo unafanyika.

Katika hatua nyingine Lwota amewataka madiwani hao na watumishi wengine katika wilaya hiyo kuanza maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kuanza kukimbizwa wilayani humo mwanzoni mwa mwezi wa Julai, 2024.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni, Jumanne Ismail alishukuru mshikamano uliopo baina ya chama na Serikali ambao unaendelea kuifanya halmashauri hiyo kusonga mbele.

Ismail alisema Aprili 15, 2024 wanatarajia kuanza kufanya mikutano ya hadhara katika kata zote wakianzia wilayani Manyoni na kisha Itigi na lengo la mikutano hiyo ni kuzungumza na wananchi kuhusu miradi yote iliyotekelezwa katika maeneo yao na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM.Katika kikao hicho cha baraza la madiwani ambacho kilikuwa na ajenda nane Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hussein Simba aliweza kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa halmashauri hiyo, Ayubu Kambi na kutoa taarifa fupi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kumpa picha halisi ya miradi hiyo ili aielewe na atakapoanza kazi ajue pa kuanzia.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Ayubu Kambi akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni, Jumanne Ismail, akizungumza.

Katibu wa CCM Wilaya ya Manyoni Maimuna Likunguni, akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Mchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Emmanuel Dyilu, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAFU) wa wilaya hiyo, Valence Kilasara akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya wafufaika wa mfuko huo.
Diwani wa Viti Maalumu, Elizabeth Kidolezi akiomba ukamilishwaji wa mabweni kwa wanafunzi wa Sekondari wa Kata ya Rungwa.
Diwani wa Kata ya Mgandu, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Martin Kapona,akisoma taarifa katika baraza hilo.

Diwani wa Kata ya Sanjaranda, Nikodemas Nkuwi, akizungumzia wanaufaika wa TASAFU na changamoto ya Tembo wanaokula mazao ya watu ambapo ameomba msaada wa kumaliza changamoto hiyo.
Diwani wa Kata ya Rungwa, Said Sudi akitoa shukurani zake baada ya kata yake kujengewa kituo cha afya ambacho Februari mwaka huu kimeanza kutoa huduma za upasuaji kwa wajawazito.
Mwenyekiti wa Wanawake wa Samia Mkoa wa Singida, Asha Mohamed Mwandala akiutambulisha umoja huo katika kikao hicho.
Waratibu wa vikao wa Halmashauri hiyo wakiwa kazini. Kushoto ni Makandaiga Magabe na Constantine Mihambo.
Naibu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Jonathan Hemed, akitoa taarifa za kamati katika kikao hicho.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Manyoni wakiwa kwenye kikao hicho.
Diwani wa Viti Maalumu, Utukufu Gwimile (kushoto) akiwa na madiwani wenzake katika kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Baadhi ya wakuu wa Taasisi za Umma wa Wilaya ya Manyoni na Itigi na wakuu wa idara wa Wilaya ya Itigi wakiwa kwenye kikao hicho.
Wakuu wa idara wakiwa kwenye kikao hicho.
Wanachama wa Wanawake na Samia Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Viongozi wa Halmashauri hiyo wakiwa meza kuu wakati wa kikao hicho.

Kikao kikiendelea. Kutoka kushoto ni Diwani wa Viti Maalumu, Amina Msita, Diwani wa Kata ya Mgandu, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Martin Kapona, Diwani wa Viti Maalumu, Utukufu Gwimile na Diwani wa Viti Maalumu, Elizabeth Kidolezi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments