Barabara Kufungwa Kwa Saa 3 Kupisha Mazoezi

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amesema Barabara ya fukwe ya Coco Beach kuelekea Daraja la Tanzanite, Agha Khan hadi Ocean Road itafungwa upande mmoja na kutumika kwa ajili ya mazoezi kuanzia saa 12 hadi saa 3 asubuhi kila Jumamosi.

Waziri Majaliwa amesema hayo leo akiwa bungeni akijibu maswali ya wabunge ambapo amebainisha kuwa barabara hiyo itafungwa ili kuwawezesha wananchi kujumuika kwa pamoja ili kufanya mazoezi kwa uhuru.

Majaliwa amesema kumekuwa na mwamko wa watu na vikundi vya mazoezi ambao hufanya mazoezi barabarani katika maeneo mbalimbali Jiji la Dar Es Salaam hivyo Serikali imeona ni vyema kuunga mkono juhudi hizo na kuhamasisha zaidi jamii kushiriki kwenye mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyo ambukiza.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments