CCM IRINGA WAWAPONGEZA WALIMU WAZALENDO

 

Katibu Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM mkoa wa Iringa, Joseph Ryata akiongea na walimu wazalendo wilaya ya Kilolo mkoani Iringa


CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimewpongeza walimu wazalendo kufundisha kwa juhudi na kumuunga mkono Rais Dr Samia suluhu Hassan katika kutekeleza ila ya CCM ya 2020/2025 kwa vitendo.

Akizungumza na walimu wazalendo Katibu Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM mkoa wa Iringa, Joseph Ryata alisema kuwa walimu wamekuwa na mchango mkubwa wa kimaendeleo kutokana na kutoa elimu kwa wote na mara nyingine kuwaelimisha wazazi umuhimu wa elimu.

Ryata alisema kuwa walimu wanaaminiwa na jamii kutokana na elimu,burasa na maarifa wanayotumia kwa jamii wanayoishi nayo kwa kuwaelimisha mambo mbalimbali ya kimaisha na kimaendeleo.

Alitumia wasaa huo kuwataka walimu kusaidia serikali kuyaelezea mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kutoka ushauri wenye hoja za kujenga kwa viongozi wa Chama na Serikali katika maeneo wanayoishi ili kuhakikisha ilani ya CCM inatekelezwa ipasavyo kwa maslahi ya wananchi.

Ryata amewapongeza walimu hao kwa umoja na uamuzi wao mzuri wa kuunda na kujiunga katika jukwaa la Walimu Wazalendo huku akisema Mwanachama au Kada wa CCM asipokuwa Mzalendo hawezi kuwa na tija ndani ya CCM na hawezi kufaidika vyema na fursa mbalimbali ndani ya Chama hicho na nchi kiujumla.

Sambamba na hilo, Ryata amewataka walimu hao kuendelea kuielimisha jamii na kusimamia maadili, misingi ya utoaji Elimu Bora na Malezi kwa watoto ambao ndio wanafunzi wao wanapokuwa shuleni.

Kwa upande wao walimu wazalendo wamekipongeza chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa kuendelea kuwapa ushirikiano na kutambua mchango wao katika jamii huku wakiomba Uongozi uzidi kuwapambania na kuzisema kero na changamoto zinazowakabili walimu katika utumishi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments