Chama kuzikosa mechi hizi Simba

Baada ya kufungiwa michezo mitatu kwa kosa la kumkanyaga mchezaji, Nickson Kibabage kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama ataikosa michezo miwili ya nyumbani na mmoja wa ugenini.

Chama ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi na kisha kuikosa tena Tabora United Mei 6 dimba la chamazi na mchezo wa tatu ni dhidi ya matajiri wa Kusini mwa Dar es Salaam Azam Fc Mei 9, 2024.

Simba wanapitia ukame wa kutopata ushindi katika michezo mitatu ya Ligi Kuu, mara ya mwisho mnyama kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi ni Machi 15, 2024 walipoifunga Mashujaa 2-0 mabao yote yakifungwa na Chama.

Tangu Machi 15 Simba imecheza michezo nane katika mashindano mbalimbali ikishinda michezo miwili pekee, vipigo vinne, na sare katika michezo miwili.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments