TIMU za Ihefu ,Yanga, na Coastal Union zimetinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kushinda michezo yao ya Robo fainali.
Ihefu imefuzu hatua hiyo baada ya kuitoa Mashujaa ya Kigoma kwa penalti 4-3 baada ya timu hizo kutoka 0-0 katika dakika 90 mchezo uliofanyika Uwanja wa Liti, Singida, huku Coastal ikifuzu baada ya kuifunga Geita Gold bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Yanga yenyewe imefuzu Nusu Fainali baada ya kuifunga Tabora United mabao 3-0 Uwanja wa Azam Chamazi, ambapo timu ya nne itajulikana Ijumaa Mei 3, wakati Azam itakapocheza na Namungo katika uwanja huohuo.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Azi Ki dakika ya 35, Kennedy Musonda dakika ya 66 na Joseph Guede dakika ya 83.
0 Comments