Makonda awapa somo watendaji Longido

ARUSHA;  MKUU wa Mkoa wa Arusha , Paul Makonda amewataka watendaji na viongozi wa ngazi zote za Wilaya ya Longido kufanya kazi kwa bidii kutimiza ahadi na maelekezo ya chama na Serikali ya Awamu ya Sita  inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Makonda ametoa agizo hilo leo wilayani Longido, ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi wilayani Longido, ziara ambayo itafanyika kwa siku sita kwenye wilaya zote za Mkoa wa Arusha.

Ameesisitiza suala la uwajibikaji na kusikiliza wananchi, huku akitaka kila mmoja kutambua majukumu yake na kuthamini kuaminika kwake na serikali, akihimiza ushirikiano kutoka kwa watumishi na watendaji mbalimbali.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marko Ng’umbi amemshukuru Rais  Samia kwa kutoa Sh bilioni 44 ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Longido.

Amesema fedha hizo zimefanikisha kupeleka huduma ya nishati kwenye vijiji vyote vya Longido pamoja na kusaidia miundombinu mbalimbali ya elimu, afya na barabara

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments