ARUSHA: MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ni jukumu la kila Mwananchi wa Arusha kuilinda heshima ya mkoa huo.
Akizungumza leo katika Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yanayofanyika kitaifa mkoani Arusha, RC Makonda amesema amekutana na makundi mbalimbali ikiwemo ‘Wadudu’(vijana wapambanaji mkoani Arusha) ambao wameapa kuilinda Arusha.
https://www.youtube.com/watch?v=ZGM8Vz840mc
“Jana tuu nimekula kiapo na wadudu, hawa wadudu ni jina na ni ‘brand’ mkoa huu una kila aina ya vijana wenye vipaji mbalimbali tumekubaliana kuitumia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kusukuma maendeleo ya uchumi wao,” amesema Makonda na kuongeza.
“Tumekubaliana, kwakuwa Mungu aliwapa nafasi ya kuwa katika mkoa huu nao watasimama kuulinda, kwahiyo usalama utalindwa na wadudu, utalindwa na polisi utalindwa na mgambo,viongozi wa dini na kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayechafua heshima ya Jiji la Arusha,” amesisitiza.
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi kitaifa yanafanyika mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais Dk Philip Mpango akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.
0 Comments