Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Mei, 2024 kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika Paris Nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa Kinara na Mwenyekiti Mwenza katika mkutano huo wa Kimataifa.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Mei, 2024 kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika Paris Nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa Kinara na Mwenyekiti Mwenza katika mkutano huo wa Kimataifa.Meneja Mkuu wa Taifa Gas Davis Deogratius akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Mei, 2024 kuhusu Kampuni yao ilivyopanga kuendeleza uungaji mkono matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
Mwakilishi wa Total Energy Getrude Mpangile akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Mei, 2024 kuhusu Kampuni yao ilivyojipanga kuendelea uungaji mkono matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
Mkuu wa Maendeleo ya Biashara na Ukuaji kutoka M-Gas Resources Ltd. Abdallah Kijangwa akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Mei, 2024 kuhusu Kampuni yao ilivyojipanga kuendelea uungaji mkono matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakiwa wamesimama kimya kwa dakika moja kumkumbuka na kumuombea Mwandishi wa Habari na Mpiga Picha Marehemu Noel Mwingila ambaye alikuwa mmoja ya Waandishi wa Habari aliyekuwa akihudhuria Mikutano mbalimbali iliyokuwa ikifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
0 Comments