NEEC Kupitia Program Ya IMASA Kuwezesha Wanawake Wa Mkoa Wa Dar Es Salaam Watakaojiibulia Fursa Za Kibiashara

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, RC Albert Chalamila (katikati) , kulia kwa RC, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) , Bi Beng’I Issa kwenye uzinduzi wa programu ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) na kushoto kwa RC, Mshauri wa Rais wa Mambo ya Wanawake na Makundi Maalum , Bi Sophia Mjema na mwanzo kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na kushoto mwisho ni Mshauri wa Uchumi wa Mkoa wa Dar, Dkt Elizabeth Mshote

Mshauri wa Rais katika mambo ya Wanawake na Makundi Maalum, Bi.Sophia Mjema akiteta Jambo na Katibu wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi Beng'i Issa wakati wa Uzinduzi wa Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia kwa Mkoa wa Far es Salaam.

Katibu mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) , Bi Beng'I Issa ( mwenye shati ya njano) na Mshauri wa Rais Mambo ya Wanawake na Makundi Maalum, Bi Sophia Mjema wakicheza baada ya uzinduzi rasmi wa programu Imarisha Uchumi na Mama Samia (iMASA) uliyozinduliwa juzi jijjni Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu.
BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limewataka akinamama wa Mkoa wa Dar es Salaam kutumia fursa za kibiashara zinazopatikana katika Mkoa huo ili kuanzisha shughuli za ujasiriamali na biashara ili kuleta matokeo chanya kwenye Familia zao na Taifa kwa ujumla.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, RC Albert Chalamila wakati wa uzinduzi wa Programu ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) katika Mkoa huo ambapo alisema kwamba kuna umuhimu kwamba wakinamama wachukue changamoto na matatizo mbalimbali kama fursa za kuweza kuinuka kiuchumi.

Alisema kwamba Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuja na programu hii ili kumuwezesha mwanamke wa nchini kutoka kwenye lindi la umasikini na anaendelea kushughulikia na mikopo ya wanawake na watu kwenye makundi maalum ili iende kwa walengwa.

“Juhudi za kila siku za shughuli za kijasiriamali ndio zitakazotutoa kimaisha na kuendelea kuchangamkia fursa za kiuchumi,” alisisitiza.

Alisema hayo jana katika unzinduzi wa program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) inayotekelezwa na baraza hilo ambapo prongram ilizinduliwa kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Tunampongeza Rais Mama Samia kwa kutuletea program hii Imarisha Uchumi na Mama Samia katika mkoa wetu, na sisi tumeipokea program hii kwa mikono miwili, na tunalenga kutekeleza kwa vitendo na lengo letu azma hiyo iweze kutimia.

Alisema Mkoa wa Dares Salaam unafursa nyingi zikiwemo za kilimo cha mbogamboga, ufugaji wa kuku, Samaki ni kwenye mabwawa ya kuchimba.

“kwa sasa mkoa huu unajipanga kuendelea kujenga masoko makubwa ya kisasa katika kila wilaya nak ama mnavyojua kwamba soko la Kariakoo linajengwa la kisasa zaidi na lipo katika hatua za mwisho,’ alisema RC Chalamila

Aliongeza kwamba Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ana ndoto za kuwawezesha wanawake wa nchini kiuchumia kwa kutaka kuwaunganisha na biashara na fursa zitokanazo na miradi ya kimkakati unayoendelea hapa nchini.

Alisema kwamba serikali ya Mkoa itaendelea kuwahamasisha wakinamama katika juhudi za kutaka wajihusishe na shughuli za ujasiriamali kwa kutumia fursa zilizopo za miundombinu ya reli, Barabara na kiwanja cha ndege kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Beng`i Issa alisema baraza lake kupitia programa ya Imarisha Uchumi na Mama Samia imekuja kuwakwamua wanawake, vijana na makundi maalumu kufanya shughuli za kijasiriamali.

`Baraza la linatambua Mkoa wa Dar es Salaam mkoa unahitaji maeneo kwa ajili ya kusindika mazao yao, kuwa na masoko (super market) ili wateja waweze kwenda kununua bidhaa zilizotengenezwa hapa nchini.

Alisema baraza limejipanga kuwaunganisha wanawake na taasisi mbalimbali ikiwemo ya Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kupata technolojia na vibali mbalimbali.

Alifafanua kwamba baraza linaprogram mbalimbali ikiwemo ya local content ili watanzania waweze kushiriki katika miradi mikubwa kama ya SGR, bomba la mafuta.

Program nyingine nyingine ni ya ufundishaji somo la ujasiriamali kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu lengo ni kuwaandaa watanzania kuwa wajasirimali na kuchangia uchumi wa taifa.

Vilevile aliwataka wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa na nidhamu ya fedha kwa kuweka katika akaunti au katika vibubu ili kuendeleza biashara zao.

Jiungeni katika vikundi vya VICOBA ili kusaidia kuweka fedha na kukopa kwa vile mnakopeshana kwa riba nafuu na kujiepusha na ukoaji katika vikundi vya kausha damu.

Serikali ina mifuko mbalimbali ya uwezeshaji mikopo lakini ili kupata mwanahitajika kufuata masharti kupata fedha hivyo kila mmoja anahitajika kukidhi vigezo na kutunza kumbikumbu ili kupata fedha.

Bi Issa alisema kwamba programu hiyo ya Imasa mmoja ya jukumu lao kubwa ni kuwaunganisha wanawake hapa nchini na fursa zilizopo.

“Moja la jukumu letu ni kuhakikisha kwamba Pamoja na sera ya serikali ya kuwawezesha wakinamama lakini ni muhimu kuhakikisha tunawaunganisha wanawake hapa kwenye shughuli zote za uchumi na miradi ya kimkakati hapa nchini,’ aliongeza

Bi Issa alisema kwamba Baraza limeanza kupeleka programu ya ufundishaji wa ujasiriamali mashuleni na walianza kuanzia shule ya msingi, sekondari na hadi vyuo vikuu.

“kwa sasa kitakwimu kuna wajasiriamali milioni 5 na 54 % ni wanawake nchini nzima na baada ya uzinduzi wa programu ni matarajio yetu wanawake wataendelea kujitokeza kwa wingi,” aliongeza.

Alifafanua kwamba kupitia baraza wameanza kuwafundisha na kuwasaidia wakinamama kuandika na kuomba zabuni kwenye halmashauri katika juhudi za kuwajengea uwezo wanawake.

Alifafanua kwamba programu hiyo inalenga kuboresha Uchumi wa wanawake, vijana , wazee, walemavu na makundi maalum ili kuweza kuwainua na kutoka kwenye lindi la umasikini.

“jambo la moja ambapo tumeambiwa na wanawake ni kwamba wajasiriamali wanataka kutegemewa maeneo ya kufanya biashara na pia wakinamama wanaomba pia kujengewa masoko ili bidhaa zao za usindikaji ziweze kuuzwa hapo hasa bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini,’ aliongeza Bi Issa

Bi Sophia Mjema ambaye ni Mshauri wa Rais Mambo ya Wanawake na Makundi Maalum, alisema kwamba tatizo la mtaji , masoko na ushirikishwaji wa watanzania kwenye shguhuli za Uchumi na ndio sababu ya serikali kutunga sera, sheria na kuandaaa mwongozo ili kuweza kumsaidia mtanzania kuweza kushiriki kwenye uchumi wa nchini yake.

“Programu hii ina waratibu wa uwezeshaji wa wananchi ambao wapo kwenye ngazi ya wilaya, halmashauri na mkoa ili kuweza kuwahamasisha wanawake waweze kujiunga na majukwaa ya kiuchumi ngazi hizo ,” alisema

Kongamano hilo pia lilishirikia Benk ya NMB na CRDB kutoa elimu ya uwezeshaji na washiriki wa wengine ni vikundi vya akinamama kama Jumuiya ya Wanawake Wakatoliki (WAWATA), Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam (JUWAKITA), Jumuiya ya wanawake Wanaohusika na Madini (TAWOMA).

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments