NEEC YAZINDUA PROGRAMA YA IMARISHA UCHUMI NA MAMA SAMIA MKOA WA MOROGORO

Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limezindua Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia katika Mkoa wa Morogoro kwajili ya kuvitambua vikundi vya kinamama na makundi mengine ili shughuli zao za kijairimali ziweze kunufaika na programa hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Adam Malima alisema hayo wakati wa uzinduzi wa programa hiyo ambayo umefanywa na NEEC kuwa uzinduzi huo ni hatua muhimu kwa mkoa wake katika kufanya watanzania kufanya shughuli za ujasiriamali kwa tija.

Mkoa wetu umepokea mradi huu wa Imarisha Uchumi na Mama Samia kwa mikono miwili,‘ na tunaahidi kufanya vizuri zaidim, alisisitiza.

Alisema ili kumkwamua mwanamke ni lazima kumpatia uwezeshaji wa mafunzo na uwezeshaji na programa hii imeanza kufanya hiyo na matokeo yake yatakuwa makubwa.

Alifafanua kwamba mkoa wao utatekeleza program ya Imarisha Uchumi ana Mama Samia kwa vitendo, na hiyo itasaidia kuwawezesha watanzania kufanya shughuli za uzalishaji.

Alisema Mkoa wa Morogoro kipaumbele chake kikubwa ni kilimo na wamejipanga kuingiza mbegu za karafuu, michikichi, cocoa na parachichi ambazo watagawa bure mbegu kama njia ya kuyawezesha makundi hayo kuzalisha na kupata utajiri

Alisema shughuli za uzalishaji mazao hayo ya kilimo na shughuli mbalimbali za kijasiriamali zitasaidia watanzania kujikwamua kivipato.

Katibu Mtendaji wa NEEC,Bi. Beng`i Issa alisema Programa ya Mama Samia inalenga kuwakwamua akinamama kupitia vikundi vyao na makundi mengine ya watanzania likiwemo la vijana na wenye ulemavu.

Mkoa huu unafursa kubwa katika kilimo kutokana na ardhi nzuri yenye rutuba na watu wake wengi wanashughulisha na kilimo na shughuli nyingine za kijasiriamali` baraza litatambua shughuli zao wanazofanya katika maeneoyao ili ziweze kupata uwezeshaji alisema.

Bi. Issa alifafanua kwamba baraza lake linawaratibu katika mikoa ambapo wanatumika katika kufanyakazi ya kusaidia makundi hayo kuingia katika kanzidata zao ili hatimaye waweze kunufaika na uwezeshaji utakaotolewa na program hiyo.

Aliendelea kusema programa hiyo imekuja kuboresha shughuli zao za kilimo na shughuli zote za kijasiriamali wanazofanya na lengo ni kuwawezesha watanzania kuwa na maisha bora.

Pia aliwataka akinamama katika shughuli zao za kijasirimalia kukumbuka kuweka akiba katika mabenki au katika vibubu ili iwasaidie kupanua biashara zao.

Katibu wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mvomero,Bi. Sebastinana Mbaga alisema ujio wa program hiyo ni moja ya hatu ya kuwamua wanawake na makundi mengine kiuchumi.

Alisema katika wilaya yao wanafanya shughuli mbalimbali za kiuchumi za kijasiriamali za kilimo, kuongeza thamani mazao ya kilimo, uchuuzi na ujasiriamali mbalimbali.

Katika uzinduzi huo baraza likuwa pamoja na taasisi za kifedha ambazo zilitoa elimu namna umuhimu wa kufungua akaunti na kuweka akiba.

 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Beng"I Issa  akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuhusiana Program  ya Imarisha Uchumi na Mama Samia na kushoto kwake Ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt.. Mussa Ally Mussa. picha na Mwandishi wetu Morogoro.
 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Bi. Beng'i Issa akizungumza na makundi ya Kinamama wa Mkoa wa Morogoro wakati wa uzinduzi wa Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia kwa mkoa huo.
 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima  akizungumza na makundi ya Kinamama namna ya kunufaika na Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia wakati wa uzinduzi wa program hiyo katika Mkoa wake.
 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Adam Malima katikati akifuatilia maelezo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi NEEC. B. Beng'i Issa (kusho)kuhusu program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia, ambayo ilizinduliwa Mkoani humo. wengine viongozi na watumishi mbalimbali wa Mkoa huo Mkoani humo.
 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Bi. Beng'i Issa katikati akiwa na makundi ya Kinamama wakati wa Uzinduzi wa Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia wakati wa uzinduzi wa Program hiyo kwa Mkoa was Morogoro.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments