RAIS SAMIA ASHIRIKI UZINDUZI WA ALBAMU YA MUZIKI WA MAMA KUTOKA KWA HARMONIZE

 Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, alipowasili katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar Es Salaam, kwa ajili ya uzinduzi wa albamu mpya ya Msanii wa Mziki wa Bongofleva, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize au Konde Boy, uliofanyika ukumbini hapo, ukipewa kauli mbiu ya #MzikiwaMama, #SamiaDay, ambapo Rais Samia alikuwa mgeni rasmi. Wengine pichani ni pamoja na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Albert Chalamila na Harmonize, ambaye pia ni Mmiliki wa Kundi la Mziki la Konde Music Worldwide.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii wa Bongo Flavour Rajab Abdul aka Harmonize mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama tarehe 25 Mei, 2024. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Mzazi wa Msanii wa Bongo Flavour Harmonize, Habiba Baisa Chivalavala wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul aka Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul aka Harmonize akitumbuiza katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Albamu yake ya Muziki wa Mama tarehe 25 Mei, 2024. 


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments