KLABU ya Yanga imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania bara maalufu NBC Premier league mara baada ya kujikusanyia pointi 72 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwa mechi zilizosalia ligi kumalizika.
Yanga Sc imefikisha pointi hizo mara baada ya kuichapa Mtibwa Sugar 3-1 kwenye mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Manungu mkoani Morogoro.
Katika mchezo huo Mtibwa Sugar ilianza kupata bao kupitia kwa Charles Ilanfya kipindi cha kwanza na kuwafanya kuongoza hadi dakika ya 60 kabla ya Kenned Musonda kusawazisha na mabao mengi kufungwa na mzize na lingine wakijifunga Mtibwa Sugar.
Ubingwa huu kwa Yanga Sc ni wa 30 katika historia tokea ligi kuanzishwa na kuwaacha mbali watani wao wa jadi Simba ambao wameshachukua ubingwa huo mara 22.
0 Comments